YANGA WAPIGWA RUNGU NA SIMBA PIA, MUKOKO NA MORRISON WAPIGWA PINI

 


NYOTA Mukoko Tonombe kiungo wa Yanga amepigwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Julai 25.


Pia Mukoko amefungiwa mechi tatu kwa kosa hilo ambalo aliliafanya na alionyeshwa kadi nyekundu ya jumlajumla.

Pia taarifa imeeleza kuwa kipa wa Yanga, Farouk Shikalo amepigwa faini ya laki tano kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi jambo ambalo ni kinyume cha kanuni.

 

 Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amepigwa faini ya laki tano kwa kosa la kugoma kuhudhuria mkutano wa Waandishi wa Habari.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kutokana na kikao cha Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichokutana Julai 27.

Pia Simba imepigwa faini ya shilingi milioni mbili kwa kosa la viongozi na mashabiki kukaidi maelekezo na kuanzisha vurugu  kwa kulazimisha kuingia mlango usio rasmi na shilingi laki tano kwa kosa la viongozi kuingia uwanjani kwa mlango usio rasmi.


Adhabu nyingine ilikuwa ni laki tano kwa Simba kutokana na mashabiki wake kuanzisha vurugu kwa askari wakati wa mapumziko na nyota Bernard Morrison amepigwa adhabu ya laki tatu kwa kosa la kinidhamu pamoja na kufungiwa mechi tatu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post