Meneja wa Stoke City Mark Hughes amefutwa kazi na klabu hiyo baada ya Stoke kuondolewa Kombe la FA kwa kulazwa 2-1 na Coventry City.
Hughes, 54, alikuwa ameongoza Stoke kwa miaka minne unusu. Lakini wameshindwa mechi tano kati ya saba walizocheza karibuni EPL.