Angel Di Maria amefichua siri Real Madrid hawakutaka acheze World Cup 2014, kisa…..


Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina aliyewahi kuichezea club ya Real Madrid ya Hispania Angel Di Mariaamefunguka na kuelezea kilichomtokea katika fainali za Kombe la Dunia 2014 akilitumikia taifa lake la Argentina.

Di Maria ameeleza kuwa alikuwa yupo radhi kuichezea Argentina lakini Real Madrid hawakutaka achezea akiwa na maumivu hivyo wakatuma barua ya kuwaagiza Argentina wasimchezeshe Di Maria kwa kuhofia kuwa ataumia zaidi.

“Ilikuwa asubuhi ya saa 5 World Cup ya 2014 nikiwa nimekaa katika meza ya wauguzi nikisubiria kupatiwa matibabu ya maumivu katika mguu wangu lakini kwa dawa za kutuliza maumivu nilikuwa na uwezo wa kukimbia bila kusikia chochote kama nikipewa dawa ya kutuliza maumivu”

“Nilimwambia muuguzi kabisa kama nimevunjika wacha nivunjike mimi sijali ninachotaka ni kucheza, doctor wa timu Daniel Martinez akaja na bahasha ndani ikiwa na barua na kuniambia Angel angalia hii barua imetoka Real Madrid, nikamuuliza wanasemaje akasema hawataki uchezo haupo katika hali nzuri”

“Moja kwa moja nikajua nini kimetokea maana kila mmoja alikuwa amezisikia tetesi kuwa Real Madrid wanataka kumsajili James Rodriguez baada ya Kombe la Dunia na wataniuza ili Rodriguez awe na nafasi kubwa ya kucheza nikamwambia Doctor naomba hiyo barua na nikaichana bila  kuifungua”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri baada ya Kombe la Dunia Real Madrid wakafanikiwa kumsajili James Rodriguez na kumuuza Di Maria kwenda Man United na baadae Di Maria akaamua kwenda kuichezea club ya PSG aliyodumu nayo kwa mafanikio.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post