SABABU TANO (5) ZINAZOFANYA MAPENZI YA MBALI YASIDUMU


Wengi wetu hujiuliza kwanini  maisha ya mapenzi ya mbali huwa  hayafiki mbali na kubaki wa kijiuliza tatizo ni nini? Wakati mwingine watu huanza kuulizanaa mchawi ni nani katika mapenzi yao. Laa hasha!! Huenda mchawi wa mapenzi yako ni wewe mwenyewe lakini hujui kwa sababu hakuna mtu ambaye ameshawahi kukueleza jambo hili na lile ndio tatizo

Hata hivyo hakuna kumbukumbu ambazo zinaonesha ni kwa asilimia ngapi ambazo wapenzi wanapenda kuwa mbali mbali japo mazingira mara nyingi ndo huwa chanzo

Katika tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba umbali humaliza kabisa mapenzi ambayo  wapenzi wengi wenye malengo ya kufika mbali huwakuta.

Lakini zipo sababu mbalimbali ambazo ukizichanganua utajua kwa nini mapenzi mengi ya mbali huw hayadumu

Wivu.

Wivu huwa ni chachu ya kupima upendo lakini ukizidi pia huwa tatizo. Wivu wa mapenzi  ukizidi husababisha kutokuaminiana  kwani kila mmoja kwa wakati wake tofauti huhisi mwenzake anamsaliti, mara nyingi hali kama hii humfanya mmoja wapo kati ya wapenzi hao wawili kuona kama mwenzake ameshamchoka na anamtafutia sababu. Ni vyema kuwa na wivu kiasi kwa mpenzi wako

Mawasiliano

Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja. Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara.

Ugomvi

Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano. Inapotokea sababu za  ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.

Kutojali

Hii mara nyingi imetajwa sana kuwa ni chanzo cha mapenzi ya mbali kuvunjika kwa sababu  tofauti mfano mpenzi wako alipokuwa karibu ulikuwa ukimpatia huduma mbalimbali kama zawadi nk, lakini anapokuwa mbali unajisahau hali hii humfanya mpenzi wako ajiulize kulikoni?

Usikivu

Nayo ni sababu ambayo ukiwauliza wengi wao ambao walikuwa na uhisiano wa mbali ukavunjika lazima atakulalamikia kwamba alikuwa hanisikilizi nachomwambia. Mfano alitaka kutoka kwenda ‘OUT’ na wenzake nikamyima lakini hajanisikiza hivyo hanifai.

Hizi huenda zikawa ni baadhi ya sababu ambazo wapenzi wengi ambao mapenzi yao hayajafanikiwa kama jinsi walivyo hitaji wamekumbana nazo.

Ili kuepuka changamoto za kutengana  na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali

2 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

  1. Nafurai sana kusoma blog hii, kweli imenisaidia. Mimi ni mkongomani, na kaa mjini Bukavu mashariki mwa DRC

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa kutembelea blog yetu

    ReplyDelete
Previous Post Next Post