Kwa matokeo hayo Yanga, itakuwa na kibarua kigumu cha kuifunga Azam FC iliyowazidi pointi mbili mbele ili kufikisha pointi 55, itapata nafasi ya pili kwa uwingi wao wa mabao na ikitokea wakatoka suluhu basi watamaliza nafasi ya tatu.
WAKATI Yanga ikiwa na kilio cha kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting, Azam FC wenye makao yake makuu Chamanzi, wanacheka kwa dharau, kuona nafasi ya pili kwao ni njia nyeupe.
Kwa matokeo hayo Yanga, itakuwa na kibarua kigumu cha kuifunga Azam FC iliyowazidi pointi mbili mbele ili kufikisha pointi 55, itapata nafasi ya pili kwa uwingi wao wa mabao na ikitokea wakatoka suluhu basi watamaliza nafasi ya tatu.
Nyota wa Yanga, Emmanuel Martin amesema ili kumaliza nafasi ya pili dakika 90 za mchezo wao na Azam FC ndizo zitakazoamua nani kategua kitendawili hicho.
"Imetuumiza sana kutoka sare ya mabao 2-2 na Ruvu, tungeshinda ingakuwa imebakia pointi moja tu kuwafikia Azam FC, ila kwa sasa tumejiongezea kazi ngumu ya kupambana mpaka tone la mwisho ili matokeo,"anasema.
Wakati nyota wa Azam FC, Mbaraka Yusuph ameonyesha kufurahia sare ya Yanga na Ruvu kwamba imewarahisishia kazi, watakapokutana nao mechi ya mwisho.
"Labda nikuambie kitu, unapomuona mtu analia basi kilio chake kuna mtu kinamfurahisha, bila shaka Yanga ndio walikuwa wahitaji kuliko Ruvu, matokeo hayo yatakuwa yamewavuruga, lakini kwetu roho kwatu na njia ya kuiendea nafasi ya pili ipo wazi,"anasema.