Messi, Ronaldo, Neymar na wachezaji wengine 55 walio kwenye hatari kukosa robo fainali kutokana na sheria hii ya FIFA


Ni rahisi sana kupata kadi ya njano katika soka siku hizi hasa baada ya kutambulishwa kwa sheria mpya ya matumizi ya Video Assistance Referee maarufu kama VAR.

Upatikanaji wa kirahisi wa kadi za njano umekuja na sheria mpya ya FIFA ya ‘Fair Play’ ambayo inaweza kuamua mshindi wa kundi ikiwa timu mbili zikimaliza mechi za makundi zikiwa zimefungana pointi. 

Kwa mfano, Belgium  na England 󐁧󐁢󐁥󐁮󐁧󐁿 wanacheza leo, ikiwa watamaliza mechi kwa sare – mshindi wa kundi huenda akaamuliwa kwa sheria ya kadi za njano. Hili linaweza linaweza kuchangia timu kuamua kupata za njano makusudi kwa malengo ya kumkwepa mshindani ambaye wangepaswa kukutana nae – suala hili likawafanya FIFA kutoa onyo kwamba wachezaji watakaofanya makosa kilazima ili kupata kadi za njano – watafungiwa.

Idadi ya kadi ngapi inaweza kumfanya mchezaji afungiwe?

Wachezaji ambao watapata kadi za njano mbili watafungiwa kucheza mchezo unaofuatia – mpaka sasa wachezaji watatu waliopata adhabu hii – ndugu yetu Yussuf Poulsen aliukosa mchezo vs Ufaransa na wachezaji wawili wa Panama, Armando Cooper na Michael Amir Murillo, wote walilazimika kukaa nje kutokana na adhabu ya kadi za njano.

Je kadi zinafutwa baada ya kuvuka hatua moja ya mashindano?

Yes – kuanzia hatua ya robo fainali, kama ilivyo kwenye Champions League, wachezaji hufutiwa kadi zao na kuendelea na hatua inayofuata bila kuwa na mzigo wa kadi za njano.

Je sheria ya kufutiwa kadi ilikuwepo kabla?

FIFA walianza kufuta kadi za njano baada ya kufika hatua ya robo fainali katika mashindano ya 2010. Kwa kufuta kadi za njano kuelekea hatua ya nusu fainali – ni kadi nyekundu pekee inaweza kumzuia mchezaji kukosa hatua ya fainali.

Wahanga wa kadi za njano waliopita?

Mwaka 2002 nahodha wa Germany Michael Ballack alipata kadi ya njano katika nusu fainali dhidinya South Korea, kadi yake ya pili kwenye mashindano.Akaenda kuikosa fainali ya kombe la dunia ambayo walifungwa 2-0 na Brazil.

Baadhi ya waingereza mpaka leo wanailaani sheria ya kadi za njano, kipenzi chao cha wakati huo Paul Gascoigne alilia kama mtoto baada kupata kadi ya njano katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani Magharibi mwaka 1990, japokuwa walishindwa kwenda fainali ambayo Gazza angefungiwa kama wangewafunga Wajerumani .

Je Messi na Cristiano Ronaldo wanaweza kukosa mchezo wa robo fainali ya World Cup?

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wote wapo kwenye hatari ya kukosa mchezo wa robo fainali …. mchezo ambao unaweza kuzikutanisha Ureno na Argentina ikiwa watavuka 16 bora.

Ronaldo na Messi walipata kadi za njano katika michezo ya mwisho ya makundi yao – vs Nigeria na Iran – na kutokana na sheria ya kadi za njano haifutwi mpaka kuanzia robo fainali hivyo wachezaji wawili wakipata kadi za njano tena katika mechi za raundi ya 16 bora.

Wachezaji wote ambao wana hatari kukosa mechi zijazo za timu zao ikiwa watapata kadi ya njano

Argentina: Marcos Acuña, Gabriel Mercado, Nicolas Otamendi, Javier Mascherano, Ever Banega, Lionel Messi

Belgium: Kevin De Bruyne, Thomas Meunier, Jan Vertonghen

Brazil: Casemiro, Philippe Coutinho, Neymar

Colombia: Wilmar Barrios, James Rodriguez

Croatia: Mario Mandzukic, Ivan Rakitic, Ante Rebic, Sime Vrsaljko, Tin Jedvaj, Marco Pjaca

Denmark: Thomas Delaney, Pione Sisto, “Zanka” Mathias Jorgensen

England: Kyle Walker, Ruben Loftus-Cheek

France: Blaise Matuidi, Paul Pogba, Corintin Tolisso

Japan: Eiji Kawashima, Takashi Inui, Makoto Hasebe

Mexico: Hector Herrera, Jesus Gallardo

Portugal: Cristiano Ronaldo, Bruno Fernandes, Adrien Silva, Ricardo Quaresma, Cedric Soares, Raphael Guerreiro

Russia: Aleksandr Golovin, Fyodor Smolov, Yuri Gazinskiy

Senegal: Gana, Salif Sane, Cheikh N’Doye, Youssouf Sabaly

Spain: Sergio Busquets

Sweden: Viktor Claesson, Albin Ekdal

Switzerland: Valon Behrami

Uruguay: Rodrigo Bentancur

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post