Unawezakuwa
mtihani wa kwanza kabisa kwenye mahusiano yao kama habari zilizolifikia
gazeti hili zikiwa na ukweli wa asilimia mia.
Taarifa
ikufikie kwamba, kuna madai kuwa penzi hili jipya la muigizaji Kajala
Masanja na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ limeingia ‘mushkeli’ kufuatia Kajala
kuhoji juu ya tatuu aliyonayo Harmonize.
Tatuu
hiyo si nyingine bali ni ile ambayo Harmonize amejichora kwenye mkono
wake wa kuume ikisomeka ‘Sarah’ yaani yule mkewe waliyemwagana miezi
kadhaa iliyopita, kabla ya kutua kwa Kajala.
“Yaani
unaambiwa Kajala kamaindi sana kuhusu hiyo kitu lakini hata hivyo
inaonekana Harmonize katumia uanaume wake kumuweka sawa.“
Amemwambia
ni suala la muda tu tatuu hiyo ataangalia namna ya kuibadili isisomeke
Sarah maana kuifuta kabisa ni ngumu,” alieleza mtu wa karibu na Kajala.
Mtu
huyo alizidi kutanabaisha kuwa, Kajala amekuwa muelewa kwani tayari ni
mtu mzima na anajua jinsi gani maisha ya mahusiano yalivyo.
“Unajua Kajala licha ya kumaindi lakini bado anarudi nyuma kidogo kifikra maana yeye sio mtoto mdogo.
Ameshakuwa na mahusiano tofauti kabla ya kuwa na Harmo.
Kajala
si unakumbuka alishaolewa kabisa na akaachana na mumewe hivyo baada ya
kuwekwa chini anaonekana kuelewa,” kilisema chanzo hicho.
Mtu
huyo alisema, kwa jinsi Harmonize alivyokufa na kuoza kwa Kajala, yupo
tayari kwa lolote kwani hataki kumpoteza hivyo jambo hilo atahakikisha
linakwisha na kumpa furaha kama aliyokuwa nayo awali.
“Harmonize
humwambii kitu kwa Kajala na ndio maana unaona ndani ya muda mfupi tu
tayari ameshamnunulia Kajala gari na hata nyumba.“Harmonize yupo serious
kwenye hili penzi kuliko watu wengi wanavyofikiria. Alimzimia kitambo
sana Kajala sema tu alikosa nafasi ya kuwa wake,” kiliweka nukta chanzo
hicho.
Jitihada
za kuwapata wawili hao ambao kwa sasa penzi lao liko moto hazikuzaa
matunda kufuatia simu zao kuita muda mrefu bila kupokelewa.Hata hivyo,
jitihada zaidi zinaendelea na tunaamini watapatikana na kuweka kila kitu
hadharani.
TUJIKUMBUSHE
Penzi
la Kajala na Harmonize limechipuka hivi karibuni na kuzua gumzo sana
kwenye mitandao hususan watu wengi kujadili suala la umri kwamba Kajala
ni mkubwa zaidi ya Harmo.Hata hivyo wenyewe wameziba masikio na
wameendeleza mahusiano yao kwa kuzunguka sehemu mbalimbali za starehe na
kutupia mapicha kama yote kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram.
Tags
CELEBRITY