TFF wamfungia Obrey Chirwa wa Yanga


Baada ya wiki iliyopita kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF kushindwa kufanya maamuzi ya kesi ya utovu wa nidhamu wa mchezaji wa kimataifa wa Zambia anayeichezeaYanga Obrey Chirwa kutokana na kushindwa kufika katika kesi hiyo.
Jumapili ya January 14 2018 kamati ya nidhamu ya TFF ilikaa na kumsikilizaChirwa kabla ya kutoa adhabu, Chirwaalituhumiwa kwa utovu wa nidhamu aliyouonesha wakati wa mchezo waYanga dhidi ya Tanzania Prisons.
Baada ya kupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kamati ya nidhamu ya TFFilitangaza kumfungia Chirwa mechi tatu, kaimu afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amethibitisha taarifa hizo“Chirwa alikiri kosa kwamba kweli ametenda kosa hilo, hivyo kamati imemfungia mechi tatu na faini ya Tsh 500,000”
Kutokana na adhabu hiyo Chirwa sasa ataukosa mchezo wa Yanga dhidi yaMwadui January 17 2018, Yanga vsNjombe Mji January 21 2018 na mchezo wa Yanga vs Majimaji January 28 2018.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post