Lissu Kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa (The Hegue)


CYPRIAN Mujura ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consulotant LTD, leo kautaarifu umma kuwa kupitia wanasheria na mawakili maarufu hapa nchini wanakusudia kumfungulia mashtaka katika mahakama ya ndani na ya Kimataifa (The Heque) Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissukwa kauli zake dhidi ya serikali.



Majura amesema hayo leo Jumatatu, Jan. 15, 2017 akizungumza na wanahabari na kusema kuwa, katika Kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na BBC wakati akihojiwa na mwandishi Victor Kenani wiki mbili zilizopita, Tundu Lissu anadaiwa kusema Tanzania kwa sasa ni nchi hatarishi kwa siasa pamoja na pamoja na wote wanaohoji utendaji wa Serikali.



“Alisema watu wanauawa hovyo wanatupwa baharini kwenye viroba, tunataka atupe uthibitisho wa madai yake hayo ndani ya siku mbili zijazo kuanzia leo,” alisema Majura.

Majura amedai kauli hizo ni hatarishi kwa usalama wa nchi, na kwamba inaondoa amani ya nchi iliyoachwa na waasisi wa Taifa hili huku akieleza kuwa mawakili wamejipanga kumfungulia Lissu mahakama za hapa ndani ya Tanzania na wengine wanajiandaa kwenda Mahakama ya Kimataifa (The Heque).

Lissu yupo nchini Ubelgiji tangu wiki iliyopita, Jan. 6 ambako amelekwa ili kuendelea kupatiwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma mnamo Septemba 7, mwaka jana. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post