Baada
ya RC Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya Vyombo vya habari na
mitandao
ya kijamii alimwita mjane huyo Ofisini kwake kisha kumkutanisha na Wanasheria
wa Mkoa na kubaini utapeli mkubwa uliotumika kuuza nyumba hiyo kutokana na watu
kufoji nyaraka ikiwemo Sahihi ya Mwenyekiti wa mtaa huku nyumba hiyo ikiwa na
zuio la Mahakama.
Aidha imebainika
kuwa hati za nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa mkopo wa Shilingi
Billion moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua kinachoendelea.
Kutokana na hilo
RC Makonda ameagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro
Mambosasa kuwakamata matapeli waliohusika pamoja kuagiza kusimamishwa mnada huo
kwakuwa ni batili huku akimsihi Mama Mjane kuishi kwa amani kwenye nyumba yake.
Kwa upande wake
mjane huyo Bi. Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa
kuwajali Wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata matatizo huku akimpongeza
Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.

Tags
kitaifa