Azam FC yaomba kuzihamisha Simba na Yanga

Klabu ya soka ya Azam FC imeliandikia barua shirikisho la soka nchini (TFF) na Bodi ya ligi (TPLB), kuomba kuhamishia mechi zake za ligi kuu soka Tanzania bara zinazohusu Yanga na Simba katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.



Akiongea leo na wanahabari msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amesema wameona warejeshe mechi hizo katika uwanja wa taifa kutokana na uwezo mdogo wa uwanja wa Azam Complex hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wachache kushuhudia mechi hizo.
''Msimu uliopita wa 2017/18 mechi nne kwa maana ya mbili dhidi ya Simba na mbili dhidi ya Yanga zilichezwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani lakini tuliona changamoto nyingi kubwa ikiwa ni idadi kubwa ya mashabiki kiasi cha kupelekewa mageti ya uwanja kuvunjwa'', amesema Jaffar.
Aidha Jaffar amethibitisha kupokea maombi kutoka klabu ya Mtibwa Sugar kutumia uwanja wa Azam Complex kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo amesema tayari wameshawaruhusu kutumia uwanja huo.
Mtibwa Sugar itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo ambapo itaanza kwa kucheza mechi yake ya awali dhidi ya Northern Dynamo ya visiwa vya Ushelisheli, mechi ambayo itapigwa kati ya Novemba 27 na 28 hapa nchini.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post