'Legend' wa Simba alia na viongozi wapya

Baada ya Simba kubadili mfumo pamoja na kupata viongozi wake wapya, mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Abdallah Kibadeni amewataka viongozi kutowasahau wachezaji na viongozi wa zamani walioitumikia Simba kwa mafanikio akiwemo yeye.




Kibadeni amebainisha hilo katika majojiano maalum na www.eatv.tv ambapo amewapongeza kwa kumaliza vyema mchakato wa mabadiliko huku akiwakumbusha kuwa kuna watu wameifanya Simba kuwa hapo ilipo hivi sasa.
''Ushauri wangu mkubwa kwa viongozi ni kutosahau kututumia watu wa zamani tulioitumikia klabu kwa nguvu zetu maana wakifanya hivyo watakosea, waangalie chochote wanachoweza kututuma wasije kuwa na Simba mpya bila watu walioifikisha hapo'', amesema.
Aidha nguli huyo wa zamani amemkumbusha pia mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji asijekusahau kuwa kuna watu wameifanya Simba iwe hivyo leo na akawatenga badala yake anatakiwa kuwaweka karibu ili kuendelea kupata mawazo yao.
Kibadeni ni miongoni mwa nyota ambao walikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichocheza nusu fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974 dhidi ya Mehalal El Kubra ya Misri. Mchezo ambao uliisha kwa Simba kushinda bao 1-0 uwanja wa taifa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post