Jorge ambaye pia ni wakala wa mfungaji huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na 'Radio Red' ya Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania
''Taarifa hizo ni za uongo, mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila tu kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia kuwa Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwahiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa'', amesema Jorge.
Messi ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa Argentina mwezi Novemba mwaka jana alisaini mkataba mpya wa kusalia Camp Nou mpaka mwaka 2021 huku gharama ya kuuzwa ikiwekwa kuwa ni € 700 milioni ambazo ni takribani shilingi bilioni 2.
Msimu huu Messi ana mabao 15 kwenye LaLiga, huku Barcelona ikiwa pointi 45, tisa juu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili ikiwa 36.
Tags
Michezo