MO AKABIDHI HUNDI YA BILIONI 20, MCHAKATO WA MABADILIKO UMEKAMILIKA

 


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,'Mo' leo Julai 30 amekabidhi mfano wa hudni yenye thamani ya Bilioni 20.

Mkwanja huo ni kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba ambao unaendelea na ulikuwa kwenye hatua za mwisho za kuukamilisha mchakato huo.

Mo ameweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana na viongozi wa Simba pamoja na mashabiki katika kutafuta mafanikio ambapo timu hiyo imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo na imetwaa Kombe la Shirikisho mara mbili.

Mbele ya Waandishi wa Habari Mo amesema:-"Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu.

Pia ameweka wazi kwamba mchakato wa mabadiliko umekamilika baada ya kupata hati kutoka FCC ya kuruhusu kumalizia mchakato.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post