Wimbo wa "Bodak Yellow" haumfaidishi Cardi B tu peke yake, kuna wengi wanaopata pesa kupitia wimbo huo ambao wiki hii umefikia kiwango cha Diamond kwenye mauzo.
Akimjibu shabiki mmoja Twitter, Cardi B alisema Kodak Black anafaidika kifedha na wimbo huo kwa sababu alichangia kupatikana kwa jina la wimbo na hata midondoko (flows), pia Cardi alipata ushawishi kuufanya baada ya kuusikia wimbo wa Kodak, No Flockin.
"Alitajwa kwenye washiriki wa wimbo (credit) na wote tunafaidika nao hadi tunakufa. Wimbo unaitwa Bodak Yellow kwa sababu." aliandika Cardi B ambaye huo ulikuwa wimbo wake wa kwanza na ulitoka June 16, 2017.
Tags
CELEBRITY