Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe kustaafu kwake kuichezea timu ya Taifa lengo siyo kustaafu kabisa bali ni kujipunguzia majukumu tu.
Hapo juzi Kapombe aliandika barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania TFF na kueleza kuwa ameamua kustaafu kutokana na majeraha.
"Afya yangu ikiwa sawa nitarejea timu ya taifa, kwa sababu mimi bado ni kijana mdogo nahitaji sana kucheza.", amesema Shomari Kapombe.
"Siwezi kwenda kucheza timu ya taifa wakati najua siko vizuri, nitashindwa kuwapa Watanzania kitu wanategemea kwangu. Wataniona sio Kapombe ambaye wanamjua, hali hiyo bado naendelea kupambana nayo.", ameongeza.
Hata hivyo tetesi zinaeleza kuwa Kapombe amefikia uamuzi huo kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania kutomzingatia katika zawadi zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa wachezaji wa Taifa Stars baada ya kufanikiwa kufuzu michuano ya AFCON.

Tags
Michezo