Mtengeneza nywele wa nyota Cristiano Ronaldo anayefahamika kwa jina la Ricardo Marques Ferreira amekutwa amefariki dunia siku ya Ijumaa katika chumba cha Hoteli huko nchini Uswisi.
Ricardo ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Caju ,amekuwa akiishi mjini Zurich kwa miaka miwili iliyopita na alikuwa akiishi katika hoteli hiyo ambayo amekutwa ameuliwa.
Ricardo alikuwa ni mtengeneza nywele (hair stylist) na mpambaji ambaye amefanya kazi na wanamitindo na waigizaji wa kike wa Ureno, pamoja na nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo. Ricardo nae anatokea katika kisiwa cha Madeira,Ureno sehemu ambayo ametokea Cristiano Ronaldo.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA