Msanii wa Bongofleva hapa nchini, Gigy Money, ameonekana kutoa dongo kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanamdharau na kumchukulia poa wakati anaanza kazi ya muziki.
Gigy Money ameieleza EATV & EA Radio Digital, kuwa ilifika hatua watu wanamsema na kumshambulia mitandaoni pia walijaribu kumchonganisha na Serikali ili mradi wamshushe chini.
"Kwa watu walioni-follow, sio kila shabiki anakupenda kuna wanaokuchukia lakini wanakushabikia vilevile, kuna watu ambao walikuwa wanasema kwamba siwezi kuimba, sina lolote na nilee mtoto tu, kwahiyo hili dongo linaenda kwa watu wote mnaochukulia vitu virahisi rahisi, walikuwa wanapenda tu mimi kukaa vile" amesema Gigy Money.
Aidha Gigy Money ameongeza kuwa, "Ilikuwa ndoto zangu kuwa maarufu, nilitaka kuwa hapa nilipo sasa hivi, watu waliniambia kwamba nitakufa, nitaishia kuwa malaya pia walikuwa wananiua sana, walijaribu kunichonganisha mimi na Serikali ili mradi iniingilie kati inishushe chini na inifungie vitu vyangu" ameongeza.