Aliyekuwa rais wa
Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani
mwezi Januari.
Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.Mrithi wake Donald Trump ni mtumiaji mkubwa wa Twitter lakini Obama hakumtaja jina.
Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.
Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.
melaumiwa kwa kutumia mtandao wa Twitter kupindukia licha ya yeye kusisitiza kuwa inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na watu wa Marekani.
Tags
Kimataifa