MUONGOZO: JINSI YA KUOMBA MKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) 2020/2021



HESLB: MAJINA YA WALIOPATA MIKOPO 2019/2020 | HESLB BATCH 1


Habari yako ndugu Msomaji wa makala mbalimbali za blogu hii. Zifahamu hatua mbalimbali za kufuata ili ufanikiwe kutuma maombi yako kwenda bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), kwa kufuata hatua hizi:
Vitu vya kuwa navyo katika hatua za mchakato wa kuomba mkopo:

1.HAKIKI CHETI CHA KUZALIWA
Cheti cha Kuzaliwa kilichohakikiwa na RITA, kama bado hujahakiki cheti chako, bofya hapa kuhakiki na gharama za kuhakiki cheti chako ni Tsh 3,000/= kwa kila cheti. Kama umefiwa na mzazi mmoja au wazazi wote wawili unatakiwa kuhakiki vyeti vyao pia ili uweze kuvitumia kama kigezo cha ziada cha kupatiwa mkopo. Bofya Hapa Kusoma Mwongozo wa kuhakiki vyeti RITA



>>Bofya hapa kuhakiki vyeti vyako (Unatakiwa kujisajili kwanza) | Unatakiwa kuingia upande wa CREATE ACCOUNT

2. KITAMBULISHO CHA MDHAMINI
Kitu cha pili cha muhimu kuwa nacho ni kitambulisho cha mdhamini ambae anaweza kuwa ni mzazi au mlezi wako, na kitambulisho kinachotumika ni kitambulisho cha MPIGA KURA au cha NIDA.

3.PICHA YA PASSPORT SIZE (YA MDHAMINI NA MUOMBAJI MKOPO)
Hiki  ni kitu kingine ambacho kabla ya kuanza kufanya process za mkopo unatakiwa kuwa nacho.

Tajwa hapo juu ni mahitaji ya awali katika kuomba mkopo.

JINSI YA KUANZA KUOMBA MKOPO
Kumbuka maombi yote ya mkopo yanafanyika katika mfumo maalumu wa maombi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu OLAS na sio vinginevyo.


Kwa wanafunzi waliosomea ndani ya Tanzania watagusa hicho kipengele cha NECTA na kwa waliosomea nje ya Tanzania au Mitaala ya Nje watabofya hapo kwenye NON-NECTA Kisha utajaza taarifa zako




1.KUJISAJILI KATIKA MFUMO WA OLAS
Hatua ya kwanza kabisa katika kuomba mkopo ni kujisajili katika mfumo huo wa OLAS, na baada ya kujisajili utapewa CONTROL NUMBER na Mfumo huo ambae utaitumia katika kutuma gharama ya kuombea mkopo ambacho ni kiasi cha Tsh 30,000/= tu. Maelekezo ya jinsi ya kulipia gharama hiyo baada ya kupata control number haya hapa: 

2. KUJAZA TAARIFA ZAKO KATIKA MFUMO WA OLAS
Baada ya kufanikiwa kujisajili na kufanya malipo utatakiwa kujaza taarifa zako za kijamii na kielimu kuanzia shule ya msingi mpaka hapo ulipofikia (Form IV au Diploma), na kuambatanisha taarifa zako katika kila kipengele husika.

3.KU-PRINT FOMU YAKO YA MAOMBI YA MKOPO
Baada ya kujaza formu yako ya maombi ya mkopo katika mfumo wa OLAS, kwa usahihii, utatakiwa ku PRINT fomu yako ili uweze kutia sahihi na kupeleka sehemu zifuatazo:
 (i) Mahakamani (Kwa mwanasheria anaetambulika na serikali)
 (ii) Serikali za Mitaa (Ofisi ya Kijiji)
 (iii)Sahihi ya mdhamini
 (iv) Sahihi ya mwombaji Mkopo

4.KU- UPLOAD FORM NA 2 NA NA 5:
Baada ya fomu yako kutiwa sahih na watu tajwa hapo juu unatakiwa kuzi upload form namba2 na form namba 5 katika mfumo wa OLAS. Baada ya kufanya hivyo unashauriwa kutoa nakala ya fomu yako yote ikiwa tayari imejazwa.

5.KUTUMA POSTA KWA NJIA YA E-MS
Hatua ya mwisho kabisa katika kuomba mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu ni kutuma fomu yako ya maombi ikiwa kamili kwenda bodi ya mkopo kwa njia ya kielektroniki ya posta (EMS) na gharama zake ni Tsh 13,500/= (kama kutakuwa na ongezeko utajulishwa huko posta).
Asante kwa kutembelea mpemba blog, kwa maoni na maswali tafadhali weka Comment yako hapo chini.


8 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

  1. kama mimi ni continues student nasemea kwa mwaka wa masomo 2022/2023 mara mtakapotangaza mda wa kutuma maombi je ni vitu gani anavyo fuata mwanafunzi ambaye ni continues na ana taka kuomba mkopo tena baada ya kukosa mwaka wa kwanza na akiwa chuoni je anaweza akajaziwa fomu yake na serikali ya kijiji ambayo ipo karibu na chuo? yaani akiwa mbali na serikali ya kijiji alipozaliwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mara nyingi unatakiwa kuweka matokeo yako ya mpaka ulipofikia, mfano upo 2nd year hivyo matokeo yako kuanzia 1st year pia unatakiwa ukajiandikishe kwa Loan Officer hapo chuoni kwenu

      Delete
  2. Thanks for your help

    ReplyDelete
  3. Habar mm nimejaribu kujaxa fomu online lakin napata changamoto kwenye applicant category mm nataka kuchoose degree lkn yenyewe inaniwekea kwenye phd/masters nafanyaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna option ya local undergraduate pale' ndiyo degree hiyo

      Delete
  4. Kutuma fomu posta no lazima

    ReplyDelete
  5. Nipo hatua za mwishoni,,, katika hile form niliyodownloaf page No,6 imeniambia nibandike picha ambayo in jina langu na Reg No. yangu katika sehemu sahihi,,, najiuliza sehemu sahihi n ipi ikiwa form inapicha nilizo upload wakati najaza online na zipo clear

    Pia naomba kujua kwenye kutuma posta nahitajika kuambatanisha vyeti tofauti na ile verification No. kutoka Rita na kitambulisho Cha mdhamini?
    (Yaani ninaweza kuweka vyeti vingine Kama Cha form four,,, degree no)

    ReplyDelete
Previous Post Next Post