Southampton hatimaye wamekiri kushindwa kumweka beki Virgin Van Dijk, 26, lakini hawatamuuza chini ya pauni milioni 70. (Sun)
Meneja wa Everton Sam Allardyce aamini kuwa mshambuliji wa Arsenal's Olivier Giroud atahamia Goodison Park mwezi Junuari.(Liverpool Echo)
Arsenal wako tayari kumpa mkataba wa muda mrefu kiungo wao wa kati Jack Wilshere 25. (Sun)
Jose Mourinho anataka kuengeza namba ya 10 katika kikosi chake cha Manchester United mwezi January. (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku Real Mdrid wakimmezea mate nchezaji huyo wa miaka 24. (Calciomercato, kupitia Daily Express)
West Ham wanammezea mate kiungowa kati wa Sevilla Steven N'Zonzi, 29, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Everton. (Sun)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amakataa kukana ofa ya pauni milioni 53 kumnunua kiunga wa kati wa Bayern Munich Arturo Vidal, 30. (Daily Mail)
Tags
Michezo