Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy, amesema anamshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pongezi alizompa, kwani ni kitu ambacho hakikutarajia.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Nandy amesema kuwa ni kitu cha faraja kuona anapongezwa na kiongozi mkubwa serikalini, hivyo kimempa faraja.
“Nimefurahi kwa sababu ni mtu ambaye ananisapoti sana, na imenipa faraja sana kwani sikutarajia, kwa sababu mi nilitumiwa kwenye group nikaiona, basi nikampigia simu nikaongea naye nikamshukuru”, amesema Nandy.
Hii Leo Naibu Spika Tulia Ackson amepost kwenye instagram yake akimpongeza Nandy kwa jitihada zake anazozifanya kwenye kazi yake ya sana ya muziki.
Tags
kitaifa