Kardinali Pengo apewa barua nzito na Waumini wake

BARUA YA WAZI KWENDA KWA ASKOFU KALDINAL PENGO


Anaandika Marcus kabwella

Tumsifu yesu kristu! Baba Cardinal sisi waamini tunakuelewa sana unaposema tumuunge mkono Mh. Sana Rais wetu nasi tupo nyuma yako na tutatii.
Ila kuna kitu huenda watu hawakuelewi, Je! Ni kwamba udhalimu unaofanywa na serikali hii wewe baba huuoni? Na kama unauona umechukua hatua gani kumsaidia Mh. Rais ili atende kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu? Angalau baba Askofu Augustine Shao wa Zanzibar amegusia kuhusu madhila yatupatayo.

Kama hukumbuki yaliyotokea mwaka huu hata moja huligusii na umekuwa kipaumbele kumpinga anaeonyesha kukerwa mfano umempinga waziwazi Askofu Severine NiweMugizi alipotoa maoni yake ukasema hayo ni maoni yake na sio maoni ya kanisa sasa hayo uliyoyasema tuchukulie ni maoni yako au ya Kanisa? Kama ni ya kanisa umeyatoa kwenye kikao gani na ni nani amekutuma? Kama ni yako binafsi mbona umekuwa mwepesi kupinga wanaotoa maoni yao?
Alphonse Mawazo kauwawa na wanaohisiwa ni wanachama wa chama tawala,makada wa Ccm NA viongoz wake wengi wameuawa NA kujeruhiwa NA watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa chadema, Ben Saanane amepotea mpaka leo haonekani, Tundu Lisu kashambuliwa mchana kweupe, ofisi za mawakili zimevamiwa, kituo cha clouds media kilivamiwa, mwandishi wa gazeti la mwananchi kapotea, Mh. Nape katolewa bastola hadharani, viroba vyenye maiti zinaokotwa kila siku baharini, kwenye chaguzi ndogo tumesikia watu wameuwawa na kuumizwa na wao ndiyo wamekamatwa na kupelekwa mahabusu, Nauli za viongozi wa chama tawala za kuwaambia wafuasi wao wawapige wapinzani kwa kuwa polisi na magereza ni yao wasiogope wataenda kuwachukulia dhamana na Mh. Rais kawaambia watendaji wake ole wake atakaemtangaza mpinzani kashinda na umeona katika viti 43 ccm wamepoteza kimoja tu lakini mkuu wa mkoa kaomba radhi maana yake kuheshimu Uhuru wa watu kuamua kama unavyotuasa waamini ni kosa.! Na mengineeeengi.

Haya yoote baba mpendwa Muadhama huyaoni au huyasikii?
Mbona hujakemea maana yanalitafuna taifa chini kwa chini. Kila mtu ameacha taaluma yake na kufuata maagizo. Polisi wakikamata mtu ananyimwa dhamana ukiuliza ni maagizo kutoka juu maana yake hawana sheria wala miongozo ni maagizo toka juu.
Sijakusikia ukikemea watu wasiojulikana,
Kuna maswali tunakutana nayo tunakoishi mbona wakati wa Kikwete hukusita kukemea kauli za viongozi ikiwemo ile aliyoisema Mbinga kuhusu uingizaji dawa za kulevya kuhusu viongozi wa dini kuhusika! Na alikuwa sahihi maana alisema Mbele yenu ili mlichukue mjichunguze na mlifanyie kazi lakini ulimshukia mtoto wa watu mpaka watu wanajiuliza ulimfanyia vile sababu ni muislam? Hata katiba mpya makanisa kwa umoja wenu mliungana na kutoa matamko yote yalisomwa makanisani tena wakati wa ibada mbona sasa kimya au sababu raisi alikuwa muislam na sasa ni mkristo tena mkatoliki? Amesema wazi hatawabolea watu wa mwanza na hata baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyume cha sheria kaziacha kisa wale walimpa na wale walimyima kura sasa hiyo kauli ingekuwa imetolewa wakati wa kikwete ungekaa kimya kweli!
Kikwete huyu namkumbuka wakati wa Ramadhani akiwa na swaum aliingia kanisani na mkewe kuliunga kanisa katika msiba wa Askofu Mayalla. Alikuja Mbinga kumsimika Askofu Ndimbo lakini hukumuacha salama hata alipoteleza kama binadamu. Mh. Magufuli mkatoliki safi tena mseminari tokea ameingia nakumbuka matokeo matatu ya kiaskofu, kuwasimikika maaskofu wa shinyanga na Geita na maziko ya Askofu wa TUNDURU-Masasi. Sikumbuki kama kuna alilowahi kuhudhuria. Lakini baba muadhama upo kimya!!!!!!
Tunaomba washauri wa Mzee muelezeni ukweli Baba Muadhama hali sio shwari baina yetu na waumini wa dini nyingine na hata Madhehebu mengine juu ya misimamo ya Cardinal.

Ushauri huu nautoa kwa Baba Askofu mkuu Muadhama Cardinal Polycarp Pengo. Kutokana na mahubiri yake nami ni muumini wa kanisa hilo tokea tarehe 25/01/1975 nilipobatizwa.

Mungu mbariki Baba Askofu wetu, Kanisa letu takatifu! Rais wetu mpendwa na viongozi waandamizi wake wote.
Mungu ibariki Tanzania.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post