Wakfu wa Nelson Mandela umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo za “Nelson Mandela”, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari Tanzania, Kenya na Burundi Disemba 27, 2017. Habari hiyo pia haikutajwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.