YANGA WALAMBA DUME, KUMPATA BEKI WA GOR MAHIA



MENEJA wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba amewaambia viongozi wa Yanga iwapo wanahitaji saini ya mshambuliaji wa Gor Mahia wa Kenya, Jacques Tuyisenge wanatakiwa watoe kitita cha dola 200,000 ambazo ni sawa na milioni 460 za Kitanzania.

Yanga imeonyesha nia ya kumsainisha Tuyisenge baada ya kumpigia simu meneja huyo kwa kumtaka ataje dau la mchezaji huyo ili wafanye mchakato wa kumsajili. Hata hivyo ukiachana na Yanga pia Simba ndio walioonekana kuanza kuzungumza na meneja huyo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye kiwango cha juu ambapo inavyoonekana mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama.

Gakumba alisema kuwa, mara baada ya viongozi wa Yanga kumpigia simu aliwatajia dau la Tuyisenge ambalo ni dola 200,000 ambapo bado hawajafikia muafaka. “Viongozi wa Yanga walinipigia walitaka niwatajie dau ninalolihitaji kwa ajili ya Tuyisenge na nikawatajia kuwa ni dola 200,000 lakini bado hawajanirudishia majibu nasubiria majibu kutoka kwao.

“Iwapo watafanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha basi nitakuwa tayari kumuachia ikiwa ni pamoja na kumuhakikishia mazingira mazuri ya kazi,” alisema Gakumba. Lakini habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kwamba aliwatajia bei ya kuwakomoa ila wakikaa mezani rasmi huenda ikapoa kwa kiasi kikubwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post