BAADA YA KUWACHANA WACHEZAJI KISA KUGOMA, HAJI MWINYI AMJIBU ZAHERA



Baada ya Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwashutumu vikali wachezaji wake jana baada ya kushindwa kufanya mazoezi kisha mishahara, Beki wa timu hiyo, Haji Mwinyi amesema hawakugoma.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Mwinyi amefunguka akisema kuwa kwa sasa wanapambana kwa ajili ya kuchukua kikombe cha ligi na hawana haja ya kugomea.

Ameeleza kuwa hawawezi kamwe kumwangusha Zahera kwani wanamuheshimu na wanathamini kazi yake ndani ya timu hivyo yanayosemwa kuwa hawakufanya mazoezi hayakuwa na uhakika.

"Hakuna ukweli bwana, sisi tulifanya mazoezi kama kawaida.

"Yanayosemwa wala hayana ukweli maana kwa sasa tunapambana kwa ajili ya kusaka ubingwa.

"Hatuwezi kumwangusha Kocha wetu kwakweli, tunamheshimu mno na hilo haliwezi kujitokeza kabisa, hatujagoma," amesema Mwinyi.

Wakati Zahera akilalamikia suala hilo, Yanga hivi sasa inapaswa kuendelea kujifua vilivyo kwani itakuwa inakabiliana na Azam FC katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumatatu ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post