TARIMBA AWACHANA SIMBA, NI KUHUSU JAMBO HILI


Mwenyekiti wa Kamati ya Maalum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbass Tarimba, ameibuka na kueleza kuwa watani zao wa jadi, Simba SC hawana wataalam wa kusaka wachezaji "SCOUTING'.

Tarimba ameeleza hayo ikiwa ni siku moja baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere, ambaye awali alihusishwa kuwaniwa na Yanga.

Kwa mujibu wa Radio EFM, kupitia Sports HQ, Mwenyekiti huyo amesema Simba wamekuwa wakisubiri Yanga wataje aina ya wachezaji ambao inawahitaji ili wawasajili kitu ambacho anakiona kwa timu hiyo kama wamekosa wataalam wa kufuatilia wachezaji.

Ikumbukwe hivi karibuni Tarimba alifunguka na kusema Kamati yake maalum itakuwa inafanya harakati za usajili wa kimyakimya ili watani zao wa jadi Simba wasiweze kujua pamoja na timu zingine ambazo zimekuwa zikiwasajilia wachezaji.

Ukiachana na Tarimba, naye Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, aliwahi kulisemea suala hilo kuwa baadhi ya klabu zimekuwa zikisajili wachezaji wanaowataja kuwa kwenye mipango nao kupitia mlango wa uwani.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post