Kauli ya Yanga Baada ya Simba Kumsajili Kagere


Wakati aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere kufanikiwa kujiunga na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili, uongozi wa Yanga nao umetoa tamko lake kuhusiana na mchezaji huyo.

Hivi karibuni kabla ya Kagere kuelekea Simba, Yanga walikuwa wa kwanza kuanza kuhusishwa kumnyatia mchezaji huyo kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha kwenye mashindano ya SportPesa Suoer CUP.

Kupitia Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa Yanga haikuwa na mazungumzo yoyote juu ya kumsajili mchezaji huyo kwani mipango yao inaenda kimyakimya.

Ten ameeleza kuwa wanachama na wapenzi wa Yanga wawe na subira kwani mpaka sasa hawajataja nani na nani wamemsajili hivyo wakati ukifika kila kitu kinawekwa hadharani.

Kikosi hicho jana kimeanza rasmi mazoezi katika Uwanja wa Polisi Kurasini, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya KAGAME yanayotarajiwa kuanza Juni 29 wiki hii. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post