Mshambuliaji wa zamani wa Man United ambaye anacheza kwa sasa club ya LA Galaxy ya Marekani Zlatan Ibrahimovic amechukua headlines leo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kitendo chake cha kumpiga kofi mchezaji uwanjani.
Zlatan alimpiga kofi Michael Petrasso katika mchezo kati ya timu yake ya LA Galaxy dhidi ya Montreal Imapact baada ya Michael Petrasso kumkanyaga Zlatan wakati anarudi nyuma.
Tukio la Zlatan kumpiga kofi Michael Petrasso alikuonekana moja kwa moja na refa, hadi alipotumia ‘Video Assistant Referee’ VAR (marudio ya video ndipo alipomuonesha Zlatan kadi nyekundu ya moja kwa moja na kumuonesha kadi ya njano Michael Petrasso na mchezo kumalizika LA Galaxy wakiwa nusu uwanjani, hiyo ni kadi nyekundu ya kwanza ya Zlatan toka ajiunge MLS.