Hatimae Arsenal imeamua kumuacha Santi Cazorla


Club ya Arsenal ya England usiku wa Jumatatu ya May 21 2018 imetangaza maamuzi magumu kuhusiana na kiungo wake wa kimataifa wa Hispania Santi Cazorla baada ya kuthibitisha kuwa imeamua kumuacha rasmi.

Arsenal wametangaza kufikia maamuzi hayo baada ya Santi Cazorla kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi kwa muda mrefu, Arsenal hadi wanafikia maamuzi hayo ni kutokana na Santi Cazorla kuwa na majeruhi toka October 2016 kwa kuumia mfupa wa nyuma ya mguu karibu na kisigino (Achilles tendon).

Cazorla mwenye umri wa miaka 33 anaondona Arsenal akiwa kadumu kwa miaka sita toka alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea club ya Malaga ya kwao Hispania na ameichezea Arsenal jumla ya mechi 180, Cazorla ameeleza kusikitishwa kwake na kuondoka Arsenal.

“Najisikia huzuni kuondoka baada ya kuwa na wakati mzuri hapa nimefurahi muda wangu kuutumia katika hii club siku zote nitakumbuka matukio yetu maalum tukiwa pamoja, Ubingwa wa FA Cup 2014 ni kitu ambacho siwezi kukisahau, najivunia kuwa sehemu ya historia ya club hii” 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post