Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC ambaye amejiunga na Simba SC msimu wa 2017/2018 na kufanikiwa kuiwezesha kutwaa taji John Bocco leo ameongea na AyoVT mambo mbalimbali kuhusiana na soka lake na maisha yake mapya ya soka ndania ya Simba SC.
John Bocco alikuwa nahodha wa Azam FC hadi anaondoka na amekuja Simba na kupewa unahodha na kuiongoza timu kutwaa taji la VPL msimu wa 2017/2018 hiyo ni baada ya kuichezea msimu mmoja, AyoTV imemuuliza John Bocco anamiss nini Azam FC?
“Bila mashabiki sisi wachezaji tunakuwa hatuna presha sana kwa hiyo tofauti ya Azam FC na Simba ni kuwa huku kuna presha ya mashabiki, kweli nilikaa Azam muda mrefu na ukikaa sehemu muda mrefu unazoea vitu vingi lakini kwa mazingira ya mpira kama mchezaji unatakiwa uwe tayari kwa kitu chochote kwa hiyo hakuna nilichomiss sababu nipo katika maisha ya mpira”