TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA 25 MAY 2018



Emre CanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEmre Can

Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 24, atajiunga na Juventus mwisho mwa mwezi huu huku mkurugenzi mkuu wa mabingwa hao wa Italia Giuseppe Marotta akisema anataka kukamilisha mpango huo ndani ya siku 10. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Manchester United wana nia kulipa pauni milioni 79 kumsaini wing'a Douglas Costa kutoka Bayern Munich. Mchezaji huyo raia wa Brazil mwennye miaka 27 yuko kwa mkopo huko Juventus na mabingwa hao wa Italia wana uamuzi wa kumsaini kabisa. (Sun)


Douglas CostaHaki miliki ya pichaBAYERN MUNICH
Image captionDouglas Costa

Kwingineko United hawama uhakika ikiwa watamwinda kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, baada ya klabu hiyo ya Italia kutangaza bei ya mchezaji huo kuwa pauni milioni 87.5 kwa raia huyo Serbia. (Mail)
Manchester City wanaandaa pauni milioni 52 kumnunua kuingo wa kati wa Napoli Jorginho. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Italia mwenye umri wa miaka 26 kwa muda mrefu amekuwa kwenye orodha ya Pep Guardiola wakati anatamfuta kiungo mpya wa kati. (Calciomercato via Talksport)


Mauricio PochettinoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMauricio Pochettino

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ana matumaini ya kuwasaini mshambulajia wa Manchester United mfaransa Anthony Martial, 22, beki wa Ajax mholanzi Matthijs de Ligt, 18, na wing'a wa Fuljham Ryan Sessegnon, 18, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano, (Mirror)
Pochettino pia atamwinda wing'a wa Cyrstla Palace Wilfried Zaha, 25, lakini the Eagles wanang'ang'ana kumweka mchezaji huyo raia wa Ivory Coast. (Mail)


Victor Wanyama
Image captionVictor Wanyama

Victor Wanyama amekana madai kuwa ataihama Tottenham msimu huu. Kiungo huyo wa kati raia wa Kenya 26, amekuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Tottenham mara nane tu msimu uliopita. (Evening Standard)
Arsenal wana nia ya kumleta kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini huko Emirates. Muitalia huyo wa miaka 21 pia analengwa na Juventus. (Sky Sports)


Nabil FekirHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNabil Fekir

Kiungo wa kati wa Lyon Nabil Fekir, 24, amekataa kukana ikiwa atahamia Liverpool msimu huu. (RTL via Liverpool Echo)
Liverpool wana matumaini ya kuafikiana makubaliano ya pauni milion 60 na Fekir baada ya faianali ya Champions League. (Mirror)
Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anataka kuwaleta wachezaji hadi saba mjini London. (Telegraph)
Aliyekuwa meneja wa West Ham Slaven Bilic huenda akawa meneja mpya wa timu ya taifa ya China. (Sun)


Slaven BilicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSlaven Bilic

Aston Villa wanataka mazungumzo ya mkataba na mlinzi raia wa Scotland Alan Hutton, 33, baada ya fainali ya siku ya Jumamosi. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Liverpool James Milner, 32, anasema anazungumza na watoto wake kwa lugha ya kihispani baada ya kujifunza lugha hiyo ili aweze kuzungumza na wachezaji wenznai wa zamani huko Manchester City David Silva na Pablo Zabaleta. (Times - subscription required)


Kiungo wa kati wa zamanni wa Chelsea Frank Lampard amefanya mazungumzo na klabu ya Derby County kuhusu kuwa meneja wao mpya. Lampard 39 sasa hayuko mbioni kuwa meneja wa Ipswich Town. (Mirror)

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post