Mdau wa Singida Unite ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema anafurahishwa na mwenendo wa ligi kuu Tanzania bara ambayo imefikia hatua timu ndogo inaweza kuifunga timu kubwa.
Mwigulu amesema tatizo linaloisumbua kigi yetu kwa sasa ni kushindwa kuwa na ushirikiano katika mashindano ya kimataifa jambo ambalo limekuwa likitufanya kuwa mbali katika mashindano ya kimataifa kiasi cha kushindwa na nchi kama Zambia.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amelilaumu shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kushindwa kutoa support kwa Yanga ambayo inasbiriki michuano ya kkmataifa.
“Nikiona timu ndogo zinaanza kucheza kwa kuajiamini kama hivi unaona Kagera Sugar inaweza kushinda uwanja wa taifa tena kwenye mechi ambayo ina sherehe, ukiona Ihefu inakaribia kuitoa Yanga, Green Warriors inatoa bingwa mtetezi naona kuna kujiamini flani kunaanza kujengwa kwa wachezaji.”
“Zamani ilikuwa timu kubwa zikipangwa na ndogo, timu kubwa inapata matokeo kabla ya mechi lakini sikuhizi mambo yanabadilika.”
“Jambo ambalo bado ni tatizo ni mwendelezo wa ubora wa mchezaji kwamba akiwa bora leo tumuone bora kesho na kuendelea iondoke ile kuoanda na kushuka, sasa wachezaji wetu unaweza ukamuona bora sana leo baada ya siku kadhaa akishasifiwa kidogo anajisahau.”
“Wakati mwingine hata timu nzima zinakosa mwendelezo wa ubora kwa mfano Mbao iliyoifunga Yanga ukiiangalia kwenye mchezo unaofuata utaona tofauti kubwa sana, timu nzima imepoteza ubora.”
“Vipaji vipo, wachezaji wanaanza kujiamini lakini shida ni kujisahau. Kuna wachezaji bado hawajajua kama mpira ni biashara nzuri watu wanajali mechi za ushabiki kwa mfano nilikuwa naongea na rafiki zangu wa Yanga hivi karibuni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Simba na matumaini ya ubingwa kupungua, wakawa wanasononeka sana wanasema tujipange kwa ajili ya msimu ujao.”
“Wanatafuta ubingwa ili wacheze mechi za kimataifa, lakini mechi za kimataifa bado wanazo lakini hawaongelei hizo wanaongelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao washindane na Simba. Hizo fikra nazo bado shida.”
“Badala ya kufikiria nafasi waliyonayo ambayo inaweza kuifanya Tanzania ikawa na timu nyingi zaidi kwenye michuano ya kimataifa lakini hiyo watu hawaiangalii, ukiangalia maandalizi ya mechi ya Yanga na Rayon Sports haikuwa na uzito kama mechi ya Yanga na Simba wakati kwa fedha na nafasi ya nchi kuwa na timu nyingi kimataifa ilikuwa ni mechi muhimu sana.”
“Zambia sasa hivi inawakilishwa na timu nne kwenye mashindano ya kimataifa kwa sababu ZESCO ilifika hadi nusu fainali, kwa mtazamo wangu kwa kundi ambalo Yanga ilipangiwa nikitarajia haya TFF waiongezee wachezani hata kutoka maeneo mengune kama ambavyo waliwahi kufanya ili Yanga ifike angalau nusu fainali nchi itanufaika kwa kupata nafasi nne jambo ambalo litaifaidisha nchi.”
“Kundi ambalo Yanga imepangwa ingekuwa watu wanaojipanga ungekuwa mwaka wa kuongeza tumu kwenye mashindano ya kimataifa lakini unaweza ukashangaa sisi tusitumie hiyo fursa lakini ingekuwa Zambia wamepangwa kundi hili wangefika nusu fainali.”