SHOMARI KAPOMBE "UVUMILIVU UMENISAIDIA"


Image result for shomari kapombe
Kiraka wa Simba Shomari Kapombe amesema uvumilivu ulimsaidia kioindi baadhi ya viongozi wa klabu hiyo walipokuwa wakimpiga ‘manenomaneno’ alipokua anasumbuliwa na majeraha.
Kapombe alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila kuitumikia Simba tangu kusajiliwa kwake baada ya kupata majeraha wakati anaitumikia timu ya taifa dhidi ya Rwanda mchezo wa kuwania kufuzu fainali za CHAN 2018.
“Nilikuwa nasikia maneno mambo mengi yanaongelewa kipindi nikiwa majeruhi lakini kikubwa kilichonisaidia ni uvumilivu na nilikuwa namuomba Mungu kila siku nirejee uwanjani.”
“Maneno yaliyokuwa yanazungumzwa niliyachukulia kama changamoto kwa sababu siku zote binadamu huwezi kwenda kwenye mstari ulionyooka kuna wakati unaenda huku na kule.”


“Najua walikuwa wanaongea kwa sababu walikuwa wanahitaji mchango wangu katika timu kwa kuwa walikuwa hawaoni mchango wangu ndio maana yalianza maneno. Nilivyolijua hilo nilikuwa nafanya mazoezi kwa bidii baada ya kurejea ili kutoa mchango wangu.”
Wakati Kapombe anauguza majera, mwenyekiti wa usajili Simba Zacharia Hans Poppe aliwahi kusema kuwa, mchezaji huyo amepona lakini hataki kucheza kwa sababu ya imani za kishirikina akiamini anarogogwa.
Mwenyekiti huyo alifika mbali zaidi kwa kusema endapo Kapombe hatarudi uwanjani kwa wakati hawataendelea kumlipa mshahara kwa sababu haisaidii timu kwa chochote.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post