Mashabiki wa Liverpool wameendelea kusafiri umbali mrefu kutoka Uingereza kwenda Kiev. Kwa ajili ya fainali ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Real Madrid, mfano mmoja alikuwa anasema ametumia siku nne akipitia Sweden, kisha anaingia Latvia, anaingia Lithuania kisha Ukraine
Mshabiki mwingine amesema anatokea mjini Liverpool akipanda Train mpaka Glasgow, pale Glasgow anapanda Ndege mpaka Palanga nchini Lithuania kisha anakodi gari kama saa tatu njiani hivi kueleka uwanja wa ndege wa Vilnius hapo anapaa kuelekea Kiev.
Steven Thompson, 33, yeye anafunga ndoa leo, amekata tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi ambapo mpango ni arejee Jumapili ili aende kwenye fungate na ambaye sasa atakuwa mkewe Bi Rachael.
Rachel amekubali mumewe aende akatimize mapenzi yake kwa mpira wa miguu lakini arejee jumapili waende fungate Australia. Sasa Steven anasema sawa huyu ameniruhusu na huenda amekasirika kiasi, ila hofu yangu ni ikiwa nitaikosa ndege ya jumapili.
Fainali ya klabu bingwa ulaya inapigwa hapo kesho, Nani ataibuka na kicheko? Christiano Ronaldo na Real Madrid yake au Mohamed Salah na Liverpool?
Tags
MICHEZO KIMATAIFA