BAADA ya tetesi kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, kwamba mwanamuziki Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake, Richard Martin ‘Rich Mavoko’, Lulu amevunja nazi na kuweka mambo hadharani.
Akichonga na Mikito Nusunusu, Lulu alisema kwamba, tetesi hizo si za kweli na zilitokana na watu kuunga baadhi ya video na picha na kuonesha kwamba wapo kwenye mahaba lakini si kweli, yupo karibu na jamaa huyo kwa sababu za kikazi.
“Mimi na Rich hatujawahi kuwa na uhusiano wowote, ni mtu wangu, tunasaidiana kwenye kazi, maana ndiye kanitungia hata wimbo wangu mpya wa Ona, kuhusu mapenzi hapana kiukweli,”