VIDEO: Sababu za Okwi kumkumbuka Mafisango katika Ubingwa wa VPL leo






Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamekabidhiwa Kombe lao la VPL msimu wa 2017/2018 baada ya game dhidi ya Kagera Sugar kumalizika kwa Simba kupoteza mchezo kwa goli 1-0, tazama Simba SC baada ya kukabidhiwa taji lao la VPL msimu wa 2017/2018.
Baada ya game kumalizika mshambuliaji wa Uganda anayeichezea Simba SC Emmanuel Okwi alionesha tisheti yake iliyokuwa na ujumbe wa kumkumbuka Marehemu Patrick Mafisango ujumbe ukisomeka “Hii ni kwa ajili yako kaka Mafisango”
Emmanuel Okwi ameeleza sababu za kuandika ujumbe huo na kumuenzi Mafisango ni kutokana na Ubingwa wao wa mwisho wa Simba waliyochukua ilikuwa ni msimu wa 2011/2012 ambapo siku kadhaa baada ya Ubingwa Mafisango alifariki kwa ajali ya gari maeneo ya Chang’ombe.
VIDEO: Wachezaji wa Simba SC baada ya kukabidhiwa Kombe la VPL



Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post