Mlinda mlango wa Mtibwa Sugar Shaaban Kado amesema msimu huu hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti aliyoyapata wakati wa maandalizi ya msimu wa mashindano.
Kado amesema kwa sasa anafurahia maisha ya Mtibwa Sugar na kuelekeza nguvu kwenye mechi zao zilizosalia VPL na kombe la TFF.
“Hii ni injury yangu kubwa ya pili kwenye soka ambayo imenikaa kichwani licha kwamba bado nacheza lakini namshukuru Mungu kwa sasa naweza hata kukimbia, hizi kazi zetu mitihani yake ndiyo hii.”
“Niliumia kwenye mechi ya kirafiki wakati tunacheza na Simba wakati wa maandalizi ya pre-season. Niliruka juu kudaka mpira nilivyorudi chini kwa bahati Mbaya Bocco alinilalia kwenye goti likageuka.”
“Niliumia sana lakini naendelea vizuri katika 100% basi nipo 80% kwa kuwa niliumia halafu ligi inaendelea kuchezwa bado nina uoga ndio kitu ambacho kinanisumbua kwa sasa hata walimu wangu wameliona hilo.”
“Naweza nikacheza lakini kuna baadhi ya matukio ya kugongana bado nayaogopa lakini naendelea kusahau yale maumivu.”