Wakati msimu wa VPL 2017/18 ukielekea ukingoni kiungo wa Mbao FC Ismail Ally (jezi namba 7 pichani) ambaye kwake ulikuwa ni msimu wa kwanza kucheza ligi kuu ameeleza baadhi ya vitu alivyojifunza pamoja na changamoto kadhaa alizokabiliana nazo.
Kwenye mechi ambayo Mbao ilipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Yanga, Ismail aliingia dakika ya 55 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ndaki Robert, Ismail amesema alifurahia kupata nafasi hiyo na alikuwa anacheza mechi kubwa kwa mara ya pili VPL na kuongeza uzoefu.
Baada ya mchezo Dauda TV ilifanya mahojiano na mchezaji huyo, iangalie video hapa chini.