Inawezekana ukawa haufahamu hili na ninajua kweli wengi hamufahamu, lakini kwa taarifa yako tu ni kwamba klabu ya soka ya Barcelona ndio klabu ya kwanza kuweka rekodi ya kuwa na mchezaji kwa kila kundi kuanzia A-H katika michuano ya kombe la dunia.
Group A. Hili ni group ambalo zipo timu za Russia, Uruguay, Misri na Saudi Arabia. Ni wazi kwamba katika timu ya taifa ya Uruguay huwezi ukamuacha Luis Suarez na ndio anaiwakilisha Barcelona hapa.
Group B. Timu za Ureno, Hispania, Morocco na Iran zipo katika Group hili. Hispania tayari wametangaza kikosi chao huku Iniesta, Alba na Busquets wakiiwakilisha Barca, Nelson Semedo na Andre Gomes nao wanatarajia kuitwa Ureno.
Group C. France, Austria, Peru na Dernmark, katika kikosi cha timu ya Ufaransa kuna nyota wawili wa Barcelona, beki Samuel Umtiti na mshambuliaji Ousmane Dembele wameitwa katika kikosi hicho.
Group D. Argentina, Iceland, Croatia na Nigeria, Lioneil Messi anakwenda Urusi akiwa na timu ya taifa ya Argentina lakini Messi atakumbana na upinzani kwa nyota mwenzake wa Barcelona Ivan Ractic anayekwenda na kikosi cha Croatia.
Group E. Brazil, Switzerland, Costa Rica na Serbia, huku wachezaji wawili wa Barcelona wapo katika kikosi hiki, yupo Philippe Coutinho lakini vilevile Paulinho ataichezea Brazil katika michuano hii.
Group F. Ujerumani, Korea, Sweden na Mexico, wakati huu ambapo Manuel Neuer hayuko fiti, golikipa namba moja wa klabu ya Barcelona Marc-Andre ter Stegen atakaa katika goli la Ujerumani.
Group G. Belgium, Panama, Tunisia, Uingereza, pamoja na kuwa majeruhi lakini Thomas Vermaelen amejumuishwa katika kikosi cha Ubelgiji, lakini Group H Yerry Mina atakuwepo kuiwakilisha Colombia.
Tags
KOMBE LA DUNIA 2018