Tarehe 8 mwezi wa sita mwaka 2002 hii tarehe waitaliano hawawezi kuisahau kabisa.
Italia iliongozana kwenda nchini Korea ya kusini kwenye michuano ya kombe la dunia. Ilikuwa na wachezaji wake wakubwa na bora duniani kwa waka Alessandro Del Piero, Christian Vieri, Francesco Totti and Pippo Inzaghi. Nyuma walisimama wachezaji nguli sana katika safu ya ulinzi kama vile Fabio Canavaro, pamoja na nahodha wao bora Paulo Maldini akisaidiana na Allesandro Nesta.
Guus Hiddink ndiye alipewa kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Korea kusini ambayo ilikuwa timu dhaifu kabisa. Hakimu wa mpambano huu alikuwa muuza madawa ya kulevya bwana Moreno mzaliwa huyu huyu wa Quito mji ambao Antonio Valencia alitorokea akiwa hana hata shilingi kumi akiwa na miaka 14.
Uwanja ulijaa takribani wakorea wote. Uwanja ule ulikuwa una uwezo wa kubeba watazamaji 40,000. Wakorea walikuwa wakipiga ngoma zao huku wakiimba “Dae Han Min guk”
Wakorea walipata tuta lakini walishinda kufunga. Kisha Vieri aliweka cha kwanza na kuwakimbilia wakorea waliokuwa wakiimba kama wamebana pua akiwaonesha ishara ya kidole mdomoni akimaanisha kaeni kimya.
Mungu sio athumani katika dakika za majeruhi watu hawa wenye pua fupi na macho ya kuvimba walipata bao la kusawazisha. Mpira ukaenda katika dakika za Nyongeza. Wakati ule mtindo wa goli la dhahabu ndilo lilikuwa kitanzi kilichikuwa kinatumika kunyonga mmoja wao.
Ngoma na makelele ya wakorea yaliwatia vijana wao wafupiwafupi na wembamba hamasa kubwa. Mambo yalikuwa moto. Waitaliano hali ilikuwa mguu wa shingo. Hakuna aliteamini kinachoendelea.
Dakika za majeruhi paaap Damiano Tommasi akaweka kambani lakini mwanaume huyu wa Ecuador Mzee baba Moreno akasema hapana braza Tommasi eeh umeotea.
Kila mchezaji wa Italia alitamani kumvunja mguu muecuador huyu.
Huyu Moreno alikuwa na roho ya kigaidi haswa. Wewe mwenyewe si unawajua watu wa kule Amerika kusini na hapo Amerika kati walivyo kibabebabe? Yaani zile sura za madawa ya kulevya ndiyo kama alivyo bwa Moreno.
Kule amerika kusini maisha yao ni ya kibabe, mtu hana gari lakini ana bastola kama zote.
Katika mpambano ule Bwana Raf Dialo mwandishi nguli wa Newstalk yeye analaumu sana mashindano ya FIFA kuwa wenyeji wa mashindano hayo wamekuwa wakibebwa bebwa sana. Goli la Tommasi halikuwa la kuotea kabisa hata kaka Steve Wonder yule mwamuziki kipofu au Mzee Reuben Kigame wasingepuliza kipenga kuashiria kuna mtu kajenga kibanda kwenye ardhi ya wakurya.
Kocha mkuu wa Italia bwana Giovan Trapattoni alitamani ammeze mwamuzi yule. Mbaya Zaidi bwana Moreno alitoa kadi nyekundu ikiwa ni kadi ya pili ya njano kwa Totti. Sasa piga mahesabu wewe ndio kocha, Mwamuzi anagomea goli la wazi kisha anamwongezea mchezaji wako muhimu kadi nyekundu.
Nimejiuliza sana Manara angekuwa muitaliano angefanyeje? Kufungwa na Kagera tu alihangaika kama Fiat inapanda mlima je hili sakata la Italia?
Nimejiuliza sana Manara angekuwa muitaliano angefanyeje? Kufungwa na Kagera tu alihangaika kama Fiat inapanda mlima je hili sakata la Italia?
Dakika ya 103 Totti alikwenda nje Daejon Stadium. Kunako dakika ya 117 kabla Moreno hajakamilisha kazi yake ya kuhakikisha Italia wanakwenda nje ya nusu fainali kijamaa kimoja kijulikanacho kama Aah Jung hwan akapleka kilio Italia. Ikumbukwe wazi kwamba ukifungwa goli kila mtu kwao. Italia wakatupwa nje ya mashindano hayo.
Mwamuzi huyu pamoja mshika kibendera wake inaonekana kama kuna njama ambazo aidha walitumwa kweli na FIFA au ni uzembe wao tu. Kwanza Moreo alitoa penati ya ajabu sana ambayo siamini kama marefa wabovu wa kiingereza wangetoa.
Sepp Blatter alikiri kuwepo kwa maamuzi mabaya katika mchezo ule lakini alikanusha vikali kuhusikana njama za kuitoa Italia katika michuano ile.
Ukijaribu hata kuangalia mchezo huu kwenye mitandao utagundua mchezo ule ulikuwa na kila sababu ya ufukunyuku. Kwanza yule Young Song alimpiga Del Piero kiwiko cha makusudi kabisa na kumtoa damu lakini wamuzi akasema twende. Chun So chaa alicheza faulo mbaya sana. Alikwenda na miguu yote kama anaua mwizi lakini mwamuzi akasema twende kazi. Kadi nyekundu ya Totti ilikua Dhahiri ni penati kwa Italia lakini mwamuzi kwakuwa alikuwa na kinoti mfukoni hakujali sana.
Huyu jamaa kwanza kila mtu alishangazwa kwa namna alivyopata nafasi ya kuchezesha kombe la dunia. Msimu mmoja kabla ya kombe la dunia kule Ecuador alisimamishwa. Liga Deportiva Universitaria de Quito dhidi ya Barcelona Sporting Club, Moreno aliongeza dakika 6 za nyongeza ambazo zilionekana kuwa nyingi.
Wakati ule alikuwa na malengo ya kutaka kugombea kwenye uchaguzi katika jimbo la Quito. Hivyo aliwabeba Quito ili kukamilisha dhamira yake. Katika mchezo ule cha ajabu mchezo ulikwenda hadi dakika 13 ambapo klabu ya kutoka mji wa Quito iliweza kupata magoli mawili katika dakika hizo.
Baada ya adhabu yake kuisha alisimamishwa tena kwa kutoa kadi nyekundu tatu katika mchezo mmoja mbazo zote zilionekana kuwa sio za kweli.
Hata hivyo aliwahi kualikwa nchini Italia kwenye kituo kimoja cha Tv alipofika alizomewa sana licha ya kwamba alilipwa pesa zake kwakutokea katika tamsha hilo.
Baadae aliamua kufanya kazi ya uchambuzi wa soka katika Tv kubwa nchini Ecuador. Licha ya kuvurunda kwa kuchezesha vibaya michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 lakini bado uchambuzi wake ulikosha wengi na kujizolea umaarufu mkubwa sana kama ilivyo kwa Shaffih Dauda. Pia alikuwa smati sana kwenye chambuzi zake unaweza kumfananisha na Geoff Lea hapa kwetu Tanzania.
Aliamua kuachana na mke wake wa hapo awali kabla ya kutoka kimapenzi na msichana aliyeonekana kuwa katoto kadogo. Kwa sasa ana umri wa miaka 48.
Mwaka 2010 kidogo angesahaulika kwenye ardhi ispokuwa tu kwenye akili za waitaliano baada ya kukutwa akiwa ambeba heroini madawa ya kulevya tumbo, makalioni na miguuni.
Inasemekana sababu kubwa za kushtukiwa ni kitendo cha yeye kuonekana kuwa na wasiwasi mkubwa alipokuwa akipita kwenye ukaguzi. Maaskari walimshuku kisha wakaamua kumkagua. Mwaka 2011 alikiri kosa hilo kule nchini Marekani.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 10 lakini wakili wake alimtetea sana mahakamani kwamba Moreno alifiliska sana na alikuwa na madeni makubwa ambayo yalitishia maisha yake.
Mbaya Zaidi mke wake alikuwa mgonjwa ambaye alikuwa hatarini kupoteza uhai wake hivyo ilibidi afanye kazi ya kubeba madawa ili kunusuru maisha ya mke wake na maisha yake kiujumla. Kifungo chake kilipungua hadi kufikia miaka 2 na nusu.
Akiwa katika Gereza la Metropolitan kule Mjini Brooklyn jamaa alianzisha mashindano ya fasheni ndani ya gereza, kisha akajpatia umarufu na fedha nyingi ndani ya Gereza. Baadae akaona mpunga ule haumtoshi akaamua kuanzisha ligi yasoka ndani ya Gereza.
Kisha baadae alipewa cheti cha nidhamu safi kabala ya kuachiwa kwa kutmikia kwa miezi 26 pekee. Hata hivyo wakili wake aliomba kifungo kile kipungue kwani maisha ya gerezani yaliathiri sana maisha yake. Jaji Edward Korman alipkea ujumbe kutoka kwa Moreno ukisema hivi “naomba san aunisamehe, kutoka kwenye uvungu wa moyo wagu. Nina matumaini kwamba ni Mungu na wewe pekee ndiyo mnaweza kunisamehe.
Jaji Kormani aliamua kumsamehe. Waitaliano bado walikuwa na kinyongo nae. Buffon alipopata taarifa za kufungwa Moreno alisema hivi.
“Sei chili di droga? Li aveva gia nel 2002, ma non nelle mutande, in corpo.” Maanake ni “kilo 6 ya unga? Mwaka 2002 alikuwa na unga lakini sio kwenye nguo yake ya makalio ila kwenye mfumo uliomtuma kutuondosha sisi”
“Sei chili di droga? Li aveva gia nel 2002, ma non nelle mutande, in corpo.” Maanake ni “kilo 6 ya unga? Mwaka 2002 alikuwa na unga lakini sio kwenye nguo yake ya makalio ila kwenye mfumo uliomtuma kutuondosha sisi”
Je mwaka huu tutegemee akina Moreno wengine? Mimi naamuamini sana Damir Skomina na atafanya vyema mno. Makala hii imedadavuliwa na kuandaliwa name Privaldinho unaweza pia kunifollow kwa ji na hilo hilo.
Tags
KOMBE LA DUNIA 2018