Majambazi Wenye Silaha za Moto Wavamia Kituo cha Mafuta na Kuiba Fedha za Mauzo


Leo April 16, 2018 stor ninayokusogezea ni kuhusu Majambazi wapatao wanne wakiwa wamevalia makoti meusi na silaha za Moto wamevamia kituo cha Mafuta cha Manjis cha jijini Arusha na kufanikiwa kupora kiasi cha Milioni 2 fedha za mauzo. 

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusufu Ilembo amesema kuwa   majambazi hao walifika eneo la tukio wakitembea kwa miguu na kuwalazimisha wafanyakazi waliokuwepo katika kituo hicho kulala chini huku wakifyatua risasi mbili hewani na kuelekea ndani ya ofisi zinapohifadhiwa fedha.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post