Michuano ya UEFA Champions League hatua ya robo fainali usiku wa April 4 2018 iliendelea tena kwa michezo miwili kupigwa, FC Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa Nou Camp walicheza dhidi ya AS Roma wakati Liverpool walicheza na Man City katika dimba la Anfield.
Game kati ya Liverpool dhidi ya Man City ndio ilikuwa inasubiriwa kwa hamu usiku huo, hii inatokana na kuzikutanisha timu zinazotoka Ligi Moja (England) kucheza zenyewe kwa zenyewe, Liverpool wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa Anfield wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Liverpool yakifungwa na Mohamed Salah dakika ya 11, Chamberlain dakika ya 21 na Sadio Mane dakika ya 31.
Ushindi huo sasa unaipa wakati mgumu Man City itakayoikaribisha Liverpool katika game yao ya marudiano itakayochezwa katika uwanja wa Etihad wiki zijazo, kwani Man City ili apindue matokeo na kuitoa Liverpool atazimika katika mchezo wa marudiano kupata ushindi wa kuanzia magoli 4-0, lakini kwa kipigo walichokutana nacho Anfield leo kimeanza kukatisha tamaa mashabiki.
Matokeo ya game ya FC Barcelona vs AS Roma