“Nimenyang’anywa gari la Serikali licha ya kuwa ni haki yangu” -Mbowe
Leo April 4, 2018 Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amesema amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge ambalo ni haki yake kuwa nalo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 4, Mbowe amesema amenyang’anywa gari hilo tangu January, 2018.
“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.” -Mbowe
“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” amesema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.
“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” -Kagaigai.