Shiloleh Amsifia Uchebe Kwenye Mambo ya Chumbani.


Mwanadada abaesifika kwa kupika chakula kitamu katika mgahawa wake wa shishi food , Shiloleh amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwaponda sana wanaume wa Dar kutokana na tabia zao za kupenda kula chipsi mayai na kuwaita kuwa hao sio wanaume halisi.

Shiloleh anasema kuwa pamoja na hayo anaona kuwa wanaume hao wanaopenda chipsi hawawezi kumpata kwa sababu mume wake sio legelege kama wanaume wa aina hiyo kwa sababu mume wake  sio mla chipsi kama mwanaume mwingine.

Akimsifia mume wake Shiloleh anasema kuwa hawezi kumfananisha mwanaume wake na mwanaume mwingine yoyote kwa sababu ya shughuli kubwa aliyonayo chumbani haifanani na mwanaume yoyote.

Shiloleh na Uchebe wameoa mapema mwaka huu na ndoa yao imekuwa ni ndoa tulivu isiyokuwa na migogoro na kuwa shiloleh anasema kuwa mume wake ni mume halisi aliyekuwa akimuhitaji siku zote.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post