UHURU KENYATTA,
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana.
Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi.
Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania.
Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Alishindwa kwenye uchaguzi huo.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi.
Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva.
Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu.
Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi
Judi Wakhungu (Mazingira) -
UfaransaCleopa Mailu (Afya) -
Umoja wa Mataifa mjini GenevaDan Kazungu (Madini) -
TanzaniaPhylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji,
Luxemburg na Umoja wa UlayaWilly Bett (Kilimo) - IndiaJacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, ParisHassan Wario (Michezo) - Austria
Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni:
Adan Mohammed - Viwanda
Amina Mohammed - Elimu
Charles Keter - KawiEugene Wamalwa - UgatuziFarida
Karoney - ArdhiFred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama
Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu)
James Macharia - Uchukuzi
John Munyes - Madini na MafutaJoseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Keriako Tobiko - Mazingira
Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma
Monica Juma -Mambo ya Nje
Mwangi Kiunjuri - KilimoNajib Balala - UtaliiPeter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki
Racheal Omamo - UlinziRaphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa)
Rashid Achesa - MichezoSicily Kariuki - Afya
Simon Chergui - MajiUkur Yattany - Leba