Ha!!Kumbe Mkhitaryan na Mourinho kulikuwa na tatizo


Kocha wa timu ya taifa ya Almernia Artur Petroysan amesema kwamba mchezaji wao wa timu ya taifa Henrikh Mkhitaryan alikuwa na tatizo na kocha wa Manchester United Jose Mourinho ndio maana akaondoka.

Petroysan anasema sio timu ya taifa tu bali raia wote wa Almernia walikuwa na furaha kubwa baada ya mchezaji huyo kujiunga na Mancheater United akitokea Borussia Dortmund lakini yaliyomtokea mtu wao hawakuyafurahia.

Mkhitaryan hakuwa akipewa nafasi ya moja kwa moja na Mourinho huku mara nyingi akikaa katika benchi la Manchester United na mara kadhaa alikosekana kabisa katika kikosi cha Manchester United.

Artur amesema wakati Mkhi akiwa United alikuwa na tatizo na kocha lakini sasa kwa kuwa yuko Arsenal wanaamini mambo yatabadilika na huenda mchezaji wao akaanza kurudi katika kiwango cha hali ya juu kama ilivyokuwa Dortmund.

Artur amekazia kwamba japo hana furaha na Mourinho lakini hana la kufanya kwani Mou ndio kucha na anajua nini alikuwa anafanya lakini sasa Waalmernia wanaamini chini ya Wenger kila kitu kinaenda kuwa sawa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post