Wachezaji 6 wanaoweza kutika timu 6 za juu EPL hawa hapa

Tunaingia wiki la mwisho la usajili wa January, lakini wakati tukielekea huko tutarajie nini katika usajili wa timu 6 za juu katika ligi kuu ya EPL?

Edin Dzeko(Chelsea). Inaongelewa sana kuhuau Dzeko na taarifa mpya zinasema tajiri Mrusi Roman Abromovich anataka kumtwaa Dzeko kwa namna yoyote ili kumfurahisha kocha wa Chelsea Antonio Conte.

Pierre Aubameyang(Arsenal). Pamoja na kurejea katika mazoezi ya Borussia Dortmund lakini mabosi wa Arsenal bado wapo nchini Ujerumani wakijaribu kufanya ushawishi kumnunua Aubameyang ambaye hata Dortmund wenyewe wameshamchoka.

Manchester City(Boubakar Soumare). Pep anatajwa kuongeza nguvu kwa kiungo huyu anayekipiga katika klabu ya Lille nchini Ufaransa na Soumare mwenyewe pia watu wake wa karibu wanasema anatamani kuwa chini ya Gurdiola.

Manchester United (Arthur Masuaku). Inaonekana kama United na City wanaigana, kwani saaa wote wanatajwa kunyemelea viungo wa Kifaransa lakini Masuaku yeye yuko EPL akikipiga West Ham na inaonekana inaweza kuwa ngumu kuwakataa United.

Liverpool (Thomas Lemar). Baada ya kuondoka kwa Phillipe Coutinho mashabiki walitarajia Liverpool watafanha usajili mkubwa haraka sana lakini hadi sasa bado hakuna kilichotokea, ila magazeti mengi nchini Ufaransa yanadai safari ya Thomas Lemar kuelekea Anfield imewadia.

Tottenham (Lucas Moura). Kuna habari zinasema kwamba Tot wameshamalizana na Moura japo hazina uhakika lakini habari ya uhakika ni kwamba Tottenham wanamtaka kwa mda sasa Moura na safari hii wanaonekana wako serious zaidi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post