STAA Lionel Messi, amekamilisha usajili wake wa miaka miwili ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain, (PSG) baada ya kukamlisha vipimo na kusaini dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambapo amebainisha kuwa ni moja ya timu yenye vipaji.
Mshindi huyo mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or aliwasili Paris, Ufaransa Jumanne kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kukamilisha usajili wa miaka miwili ambapo dili lake ni Euro milioni 25 kwa mwaka ukiwa na kipengele cha kumuongezea mkataba pamoja na bonasi.
Messi atavaa jezi namba 30 ndani ya PSG, ambayo ilikuwa ni namba yake ya kwanza kuivaa alipokuwa ndani ya Barcelona mwaka 2003 na mpaka anasepa alikuwa anavaa jezi namba 10.
Messi mwenye miaka 34 alitumia jumla ya miaka 21 ndani ya Barcelona na alisaini dili la miaka mitano kwa ajili ya kubaki hapo lakini timu hiyo ilieleza kwamba dili lake limekwama kutokana na suala la uchumi pamoja na vikwanzo ambavyo vimewekwa.
Baada ya kusaini dili hilo Messi amesema kuwa ninatarajia kuanza ukurasa wa maisha mapya ndani ya PSG. Ni kwa ajili ya timu ili kuweza kutimiza mahitaji yake.