Maswali Unayotakiwa Kujiuliza ili Kubaini Kama Mpenzi Uliyenaye ni sahihi



Inabidi kwanza wewe uwe ni mtu ulie sahihi  ndio utakapopata mtu sahihi , huwezi kupata mtu sahihi ikiwa wewe sio sahihi, au unaweza kupata mtu sahihi lakini wewe ukawa sio sahihi. ina maana kwamba lazima kwanza wewe uwe ni mwenye kujipenda ndipo utapenda na wengine

Pia ujifunze  kuwa mtu mkamilifu ili uje kupata mtu alie mkamilifu. kwa hio inabidi uwe na maswali mengi kabla hujaanza kuchukua maamuzi ya kutafuta mtu sahihi.Jiulize  , umekamilika au ni tamaa tu inakupeleka kutafuta mtu wa kukukampani.?

kama nia yako ni kupata mapenzi  tu , basi hapo bado  hujakamilika, lazima uwe na kazi kubwa ya kufanya ndani ya moyo wako kabla unahitaji kupata kazi ya kujifunza  kujipenda , na kujifunza majukumu ya kupenda wengine, uwe na hisia za kujisikia mkamilifu na usalama  za namba moja, yaani kupata na kutoa.

jiulize maswali yafuatayo.
1. Je ni mtu anyethubutu kujali, na ni mtu mwenye huruma na uelewa na mtu wa kukubalika na anakubali jinsi ulivyo. kukosekana kwa  uelewa  ni dalili ya moja kwa moja kuwa   sio sahihi

2. Je anajitahidi kulazimisha ili awe sahihi?
unaweza kuwa ,mnafanya vitu kwa pamoja , lakini bado unaona kama kuna upungufu fulani kwako huyomsio mtu sahihi kwako, hata ukijitahidi vipi huwezi kufika mbali nae.

3. Je mtu ulie nae ni muwazi kiasi cha wewe kujifunza kitu kwake?
mtu muwazi ni rahisi kjifunza  kujua kama anajipenda na kuwapenda wengine, lakini mtu wa kificho ni vigumu kujua , na hutaweza kujifunza kitu kwake. uwazi ni chombo  cha msingi sana katika mahusiano yeyote. hata kama kuna migogoro ni rahisi kurekebisha baina yenu . lakini watu wenye kificho ni ngumu hata kama kuna migogoro wanakuwa na hasira , hufoka , huhamaki, wanakuwa na hisia kali za kimwili zaidi. kwa hio sio sahihi.

4. Mnashirikiana katika kipato chenu?
mnakubaliana katika matumizi?, uzazi, kula  manunuzi ya vitu, mazoezi,usafi na kuwajibika kwa pamoja  na mnaelewana?.

5. Unapata zile hisia  za msingi , zile cheche  zinazokuvuta  kwake? unapenda kuwa karibu nae? unapenda jinsi alivyo?
Inawezekana ana harufu fulani hupendi,  kama huna hizi hisia ndani ya miezi 6 ya kuwa na huyo mtu basi hakufai, uelewe huyo ni rafiki tu wa kupita hawezi kuwa mwenza wa maisha .

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post